Breaking News
recent

Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma yafanya upasuaji wa kwanza kupandikiza Figo

Taarifa kutoka Dodoma kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa ni kwamba wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kwanza wa kupandikiza figo kwa mgonjwa Elias Yaredi wakishirikiana na madaktari kutoka Japan hapo jana na mgonjwa na aliyejitolea figo wote wawili wanaendelea vizuri.

Mpango huo wa kupandikiza figo utakuwa ni endelevu na baada ya miezi sita wana mpango wa kuwafanyia wagonjwa zaidi ya mmoja.

Gharama za kufanya upasuaji huo unafanywa gharama ya Tsh Miliion 22 ukilinganisha na upasuaji kama huo nje ya nchi wa zaidi ya Tsh Million 70.

Uongozi wa hospitali unamshukuru Rais Magufuli kwa kufanikiwa kupelekewa vifaa vya kisasa katika kuboresha upasuaji wa upandikizaji figo.


No comments:

Featured post

ADVANCED ENGENEERING MATHEMATICS

Powered by Blogger.