Breaking News
recent

Bunda: Mwili wa Samson Josiah, mmiliki wa mabasi ya Super Sami waokotwa mto Ndabaga kwenye Kiroba

Mwili wa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah unaodaiwa kukutwa mtoni ukiwa umefungwa kwenye mfuko.

 ​IMG_20180315_013638.png


Mwili wa Mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah umekutwa katika mto Ndabaka eneo la Bunda /Lamadi

Taarifa kutoka vyanzo vya habari zinasema kwamba mwili wa Samson Josiah umeokotwa na wavuvi wa samaki leo jioni Jumatano Machi 14,2018.

Watu wa karibu na marehemu wanasema mwili uliookotwa ni wa Samson Josiah.

Miongoni mwa habari zilizoteka vyombo vya habari Tanzania tangu Machi 9, 2018 hadi ni kuhusu kupotea kwa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah kwa zaidi ya wiki mbili sasa. Soma => TANZIA: Mmiliki wa mabasi ya Super Sami akutwa amekufa na gari lake kuchomwa moto Serengeti

Mapema ilielezwa kuwa gari yake ndogo aliyokuwa akiitumia aina ya Toyota LandCruiser ilikutwa imechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyoko mkoani Mara siku ya Machi 9, lakini yeye mwenyewe alikuwa hajapatikana.

Kwa mujibu wa familia ya Bwana Josiah, ambayo inaishi mkoani Mwanza, ilidai kuwa siku ya kupotea kwa Josiah ambayo ni February 27, majira ya usiku, Josiah alimpigia simu mkewe na kumwambia kuwa atarudi nyumbani na mgeni, na hayo yakawa mawasiliano yao ya mwisho.

Mabasi ya Super Sami yanafanya safari zake kuanzia mkoa wa Mwanza, kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa pamoja na Kagera.

Chanzo: Muafrika Halisi blog

=====

Jeshi la Polisi mkoa wa Kipolisi Mara, limetoa taarifa rasmi juu ya kuokotwa kwa mwili wa mfanya biashara na mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah , ambaye alitoweka na mwili wake kuokotwa mtoni hapo jana.

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara Jafari Mohamedi, amesema hapo jana walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuhusu kuokotwa kwa kiroba chenye mwili ndani, na walipokifungua na kuita watu kutambua, ndipo alipojulikana kuwa ni mwili wa mfanya biashara huyo anayeishi mkoani Mwanza.

“Jana jioni tumeweza kupata mwili wa marehemu huyu Samson Josiah ambaye ni mmiliki wa mabasi ya Super Sammy anayeishi Mwanza, kwamba kuna mwili umeonekana katika mto ambao unatenganisha mkoa wa Mara na mkoa wa Simiyu unaoelekea mbugani Serengeti, wananchi waliona kiroba kimefungwa kinaelea, kikavutwa wakajulishwa polisi kufungua ndani wakakuta mwili wa marehemu, kwa sababu tulikuwa na taarifa za utafutaji na mashaka juu ya kutoweka kwake, tukajulisha ndugu hao na wakatambua mwili wa marehemu”, amesema Kamanda Mohamedi.

Kamanda Mohamedi aliendelea kwa kueleza kwamba marehemu alitoweka kuanzia tarehe 27 mwezi wa pili ambapo aliondoka mkoani mwanza, na ndugu zake walisema kuwa aliaga anaenda Simiyu kwa shughuli zake za kibiashara na kuna mtu anamdai na akapotea tangu siku hiyo, na gari yake aliyotoka nayo Mwanza kukutwa imechomwa mtoto maeneo ya Serengeti mnamo tarehe 8 hadi kuteketea kabisa.

Imeelezwa kwamba kwa sasa mwili huo umehifadhiwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara kwa ajili ya postmoterm, na baadaye utatolewa kwenda kuzikwa, na mpaka sasa watu wanne wameshikiliwa kufuatia tukio hilo, upelelezi bado unaendelea

No comments:

Featured post

ADVANCED ENGENEERING MATHEMATICS

Powered by Blogger.